GUARDIOLA AIRUSHA ROHO BARCA

BARCELONA, Hispania
KIOCHA wa Barcelona, Pep Guardiola bado hajaamua kama ataendelea kuifundisha klabu hiyo Catalan yenye zali naye la mataji au la.
“Sijaamua chochote,” alisema Guardiola jana. “Kama nimeamua, rais angekuwa anajua.”
Guardiola ameshinda mataji 13 kati ya 15 tangu aanze kuinoa Barcelona mwaka 2008, yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa na matatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Hispania.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu na kusuasua kwake kusaini mkataba mpya inaelezwa anataka kuiacha klabu hiyo ikiwa juu.
Rais wa Barcelona, Sandro Rosell alisema Desemba alitumaini Guardiola angeamua kuendelea na kazi.
“Anafahamu anaweza kufanya anachotaka, uamuzi anao mwenyewe,” alisema Rosell. “Tutafanya yote tunayoweza ili asiseme hapana.”
Kocha wa Athletic Bilbao, Marcelo Bielsa karibuni ametajwa kama mtu anayefaa kurithi mikoba yake na Guardiola amesea Muargentina huyo atakuwa chaguo zuri.
Guardiola amejibu swali kama atakwenda kumrithi Alex Ferguson  Manchester United, akisema babu huyo mwenye umri wa miaka 70-kutoka Scotland ataendelea na kazi kwa miaka michache.
Barcelona inaikaribisha Osasuna kwenye Kombe la Mfalme hatua ya 16 bora leo, wakati msimu wa Ligi Kuu utaendelea mwishoni mwa wiki.
Guardiola alisema ataamua leo kama mshambuliaji wake nyota, Lionel Messi, ambaye alianza mazoezi na kikosi hicho jana kama atacheza leo na Osasuna au la.

Comments

  1. Dada upo shapo kweli yani pamoja sana Kheri ya mwaka Mpya

    ReplyDelete

Post a Comment