ENEO LITAKALIJENGWA UWANJA WA KISASA SIMBA LAVAMIWA

WAKATI mchakato wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu ya soka ya Simba ukiendelea, baadhi ya watu wamevamia eneo linalotarajiwa kujengwa uwanja huo na kujenga nyumba za kuishi.
Mmmoja ya viongozi wa Simba alisema jana kwamba baadhi ya viongozi wa timu hiyo walitembelea eneo hilo lililolpo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kukuta hali hiyo hali ambayo iliwashangaza.
Alisema kinachioshangaza ni wavamizi hao kuendesha ujenzi ilihali klabu imeshalipia kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Wizara ya Ujenzi na kubakisha deni la shilingi milioni 80.
Aliongeza kuwa wajumbe watatu wa Simba akiwemo Katibu Mkuu wa klabu hiyo Evodious Mtawala walikuta nyumba hizo zimejengwa katikati ya uwanja huo huku wahusika wakidai eneo hilo ni mali halali.
Kutokana na hali hiyo, uongozi umeanza jitihada za kukiokoa kiwanja hicho ikiwemo kutoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam na sehemu nyingine zinazohusika.
Hali hiyo inaonyeshja kuwa taarifa za kuhusiana na uwanja huo zilizokuwa zinatolewa hivi karibuni zilikuwa za kuweka sawa wanachama lakini ukweli ni kwamba uongozi ulichelewa kulipia ndiyo maana imefikia hatua hiyo.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHJanuary 21, 2012 at 5:39 AM

    MAUMIVU YA KICHWA HUANZA POLE POLE!NILISEMA MIMI HAPA,ADEN KAKANGU YULE NAMJUA,TAMTHILIA YETU YA UWANJA WENYE MADUKA IMEANZA KUNOGA!ILA NADHANI WANYAMA MMEONA MAMBO YA NCHUNGA PALE JUU,WATU LEO WAMETIA MIKONO KWENYE NYARAKA KIMYA KIMYA BILA MAYOWE,TENA NA KAMPUNI YA KIZAWA BILA KULETA "WATURUKI"

    MDAU WA BOMBA, REVERE MASACHUSSETTS,USA

    ReplyDelete

Post a Comment