CHAZ BABA AACHIA MPYA NDANI YA MASHUJAA BAND

NYIMBO Mpya wa mwanamuziki mpya wa bendi ya muziki wa dansi nchini Mashujaa Band Charles Gabriel, Charlz Baba' umeanza kusika katika vyombo mbalimbali vya radio hapa nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana Charlz Baba alisema hiyo ijulikanayo kama Ungenieleza ndiyo nyimbo yake ya kwanza katika bendi hiyo ambayo anaamini itasikika na kukubalika kwa wadau mbalimbali wa muziki hapa nchini.
Alisema licha ya kutoa kibao hicho anaharakati ya kutoa kitu kingine ambacho ndani ya wiki mbili nacho kitakuwa tayari kuwa masikio mwa watu.
Charlz Baba alisema  ndani ya miezi mitatu ana uhakika wa nyimbo tatu kukamilika ikiwa na hata video zake kutengenezwa.
"Hiki cha kwanza yarai kipo kwenye radio kitaanza kukika hivi karibuni na nina uhakika wadau wa muziki watakubali kazi yangu hii ambayo nimeimba kwa kushirikiana na wanamuziki wenzangu wa Mashujaa Band"alisema Charlz Baba.
Alisema wapo vizuri na wanamuziki wenzake wa bendi hiyo hivyo ana uhakika wa bendi yao kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
Charlz Baba bendi yao kesho itakuwa ndani ya kumbi wao wa nyumbani wa Business Park Kijitonyama Dar es Salaam.

Comments