CAVANI AIPELEKA NAPOLI NUSU FAINALI ITALIA, INTER KWAHERI

MABAO mawili aliyofunga Edinson Cavani yalitosha kuitupa nje Inter Milan katika michuano ya Kombe la Italia jana, Napoli ikiibuka na ushindi wa 2-0 na kutinga Nusu Fainai, ambako itakutana na  Siena.
Cavani alifunga kwa penalti dakika ya 50 na lingine dakika ya mwisho. Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2003  Inter inashindwa kutinga Nusu Fainali.

Comments