CAF YAOMBWA KUSOGEZA MECHI ZA SIMBA,YANGA

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limeandika barua kwa Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) likiomba kusogezwa kwa mechi za marudiano za hatua za awali kwa timu za Simba dhidi ya Kiyovu ya Rwanda na Yanga dhidi ya Zamalek ya Misri kutoka Machi 2 na 4 hadi Machi 9 na 11.

Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah,amesema kwamba hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Msumbiji itakayopigwa nchini Februari 29 kwani ni vigumu kwa shirikisho la soka duniani (FIFA) kubadili kalenda yake na hivyo si busara kwa timu hizo kukosa kutumia wachezaji wake kwenye mechi hizo muhimu.
“Nadhani kwa mechi ya Stars kuchezwa Februari 29 halafu tena vilabu vinakuja kucheza siku tatu amna nne baadaye si jambo zuri, tungependa vilabu vipate nafasi ya kufanya maandalizi ya pamoja walau hata siku saba na ndiyo maana tumeomba mechi zao za marudiano zisogezwe,”Alisema Osiah.
Simba na Kiyovu zinazoshiriki kombe la Shirikisho zitacheza mechi yao ugenini huku Yanga na Zamalek zinazoshiriki klabu bingwa ya Afrika zitarudiana huko Misri.

Comments

  1. VIPII DADAA HABARI ZA SIMBA NA AZAMU NGAPI NGAPI? ... AU UJAZIPATA....ILA ZA YANGA UCHELEWAJI KUWEKA.....SAMAHANI HAPA NIMEANDIKA COMMENT CUZ SIONI PA KUANDIKA...ILA UJUMBE UMEKUFIKIA
    MDAU
    MBEBA BOX WA NORWAY TANGU 2005

    ReplyDelete
  2. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHJanuary 11, 2012 at 5:06 AM

    HIVI MWANANGU KWANINI KILA WAKATI TIMU YA TAIFA INAPENDA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI NA NCHI HIYO HIYO?MBONA NCHI ZIKO KIBAO TU?

    MDAU WA YANGA BOMBA!

    REVERE,BOSTON,MASACHUSETTS,USA.

    ReplyDelete

Post a Comment