BREAKING NEWS:CHARLZ BABA AJITOA TWANGA PEPETA


MWANAMUZIKI mahiri wa bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta' Charles Gabriel 'Charlz Baba' ametangaza rasmi kujiondoa katika bendi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, nyota huyo ambaye amekuwa mmoja ya wasanii mahiri wanaiweka katika matawi bendi hiyo kongwe, alisema ameamua kujiwewka kando kutokana na kutokuwa na mkataba wa kazi tangu ajiunge nayo mwaka 2005.
Alisema kwa sasa atakuwa akifanya kazi chini ya usimamizi wa meneja wake mpya Benard Msekwa huku mambo mengine juu ya mustakabali wa kazi yake hiyo ya kisanii ukiwa juu ya meneja huyo.
"Bada ya kujitoa Twanga kwa sasa nitaelekeza nguvu zangu katika kuandaa albamu yangu binafsi na mambo mengi juu ya kazi yangu hii yatakuwa chini ya meneja wangu mpya ambaye atajua nitakwenda wapi",Alisema

Comments