SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga majina
matano kati
ya 30 ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi ya
kimataifa ya mchezo
huo iliyopangwa kufannyika Januari 16 mwaka huu.
BFT imewakata washiriki hao
baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)
kuwataka BFT kupunguza idadi ya
washiriki kutokana na hasara
iliyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya
awali iliyokuwa
ifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana.
TOC ambayo
huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzuku
inayotolewa na Kamati
ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshe
kozi hiyo tangu mwaka jana
lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wa
kozi hiyo kutoka nchini Algeria
kuingia mitini.
TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka
nje ya
Dar es Salaa kutoka katika fungu la pesa za kuendeshea kozi
hiyo
hivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale
waliofanya
utovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa
kilichobaki
kutosheleza mahitaji wa kozi itakayoendeshwa Januari 16 mwaka
huu.
Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga
alisema
idadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana
na
bajeti waliobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matano
ya
washiriki walioachwa .
Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni
mpiga picha wa
Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la
Maisha
ambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord
Ngumbi,
Moses Lema, Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es
Salaam).
Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria
Mwaseba
(Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee
(JKT
Mbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso
(Magereza
Kigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari
(Tanga).
Wengine ni Mohamed Hashim (Polisi Dar es Salaam), David
Yombayombam,
Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ), Mazimbo Ally, Rogated Damian
na
Fatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban (Magereza Dar
es
Salaam).
Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf
kutoka
Shirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana
na
makamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe.
Kozi hiyo itafanyika latika
shule ya Sekondari ya Filbert Bayi Kibaha
Mkoani Pwani na itafikia tamati
Januari 24 mwaka huu.
Comments
Post a Comment