BASENA KUISHATAKI SIMBA CAF, FIFA


ALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya Simba, Mganda Moses Basena amesema atapeleka madai yake dhidi ya klabu hiyo katika ngazi za juu zaidi akianzia Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) na ikishindikana hadi shirikisho la soka duniani (FIFA).
Basena amefikia hatua hiyo kufuatia Shirikisdho la Soka Tanzania (TFF) baada ya klabu yake ya Simba kusimamisha mkataba wake yaliwasilishwa mbele ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji.
Juzi TFF ilitoa maamuzi ya suala  la Basena  liendelee kati yake na  Simba huku ikiwataka kukaa pamoja ili waweze kulipatia ufumbuzi, lakini Simba ilibaki na msimamo wa kutokuwa na majadiliano zaidio na Basena huku ikisisitiza kuwa imeshavyunja mkataba naye.
Licha ya Basena kuwa na mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, Kamati ilibaini kuwa hauwezi kufanya kazi (functional) kwa vile kocha huyo hakuwa na kibali cha kufanya kazi nchini (work permit).
Hivyo kisheria hakukuwa na mkataba kwa vile ili Basena aweze kuitumikia Simba ni lazima awe na kibali cha kufanya kazi nchini. TFF ilikataa maombi ya Simba kuiandikia barua Idara ya Uhamiaji kuthibitisha barua ya kumuombea work permit baada ya kocha huyo kushindwa kuwasilisha vyeti vyake vya ukocha.
Kwa vile Simba imeshaajiri kocha mwingine (Milovan) kwa mkataba wa miezi sita na kupatiwa kibali cha kufanya kazi nchini, ufumbuzi wa suala la Basena unabaki kuwa kati ya klabu hiyo na kocha huyo.

Comments