AZAM FC-VPL KAMA MAPINDUZI CUP

MABINGWA wa kombe la Mapinduzi Azam FC wamesema moto waliouwasha kwenye michuano hiyo iliyomalizika Januari 12 Visiwani Zanzibar wataundeleza katika duru la pili la Ligi Kuu soka Tanzania Bara linaloanza jioni ya leo kwa nyasi za viwanja vinne tofauti kuwaka moto.
Kocha mkuu wa Azam Stewart Hall amesema kwamba kikosi chake kwa sasa kipo imara kwa kushiriki ligi hiyo ambapo timu yake itaanza rasmi Januari 25 kwa kukwaana na African Lyon.
Amesema michuano ya Mapinmduzi imeipa hamasa timu yake ambayo kadiri siku zilivyokwenda kikosi chake kilikuwa kikiiamarika na matyokeo yake kutwaa ubingwa.
"Napenda niwaeleze kuwa hili ni duru letu Azam kwani vijana wangu wamepania na kutwaa ubingwa wa VPL", Alisema

Comments