AFRICAN LYON ZUNGUMZENI UKWELI-TFF


KATIBU mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF)Angetile Osiah (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na malalamiko yalitotolwa jana na kkabu ya African Lyon ambapo amesema kuwa klabu hiyo inaficha ukweli.
Angetile akifafanua zaidi alisema suala la fedha (shilingi mili5.5)za zawadi ya timu yenye nidhamu wanazosema wanadai si kweli kwani walikubaliana zilipwe kwa mdau wa michezo nchini (Kassim Dewji) ambaye aliwakopesha kiasi hich cha fedha.
Kuhusiana na suala la Mbwana Samatta, Osiah alisema waliwandikia barua ya kuwaita ili kuongelea kama Lyon walivyoomba lakini hakuna hata kiongozi mmoja aliyejitokeza kwa ajili ya kukutana nao.

Comments