ZANZIBAR HEROES YANUSA ROBO FAINALI CHALENJI

Zanzibar Heroes, jana ilizinduka na kuishindilia Somalia mabao 3-0 katika mechi ya Kundi B ya michuano ya CECAFA Challenge Cup inayoendelea kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Heroes walionesha tangu mwanzo kuwa na uchu wa mabao ambapo iliwachukua dakika sita tu, kujipatia bao lililofungwa na Suleiman Kassim ‘Selembe’ kwa shuti akiitendea haki pasi ya Amir Hamad Omar.
Hadi mwamuzi Hudu Munyemana anapuliza filimbi ya mapumziko, Zanzibar ilitoka kifua mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili, Heroes waliingia kwa kasi na kupachika bao la pili dakika ya 50, mfungaji akiwa Amir Hamad Omar akimalizia mpira uliotemwa na kipa Khalid Mursal baada shuti la Selembe.
Heroes waliendelea kutawala mchezo ambapo dakika ya 71 shuti la Abdulham Gulam liligonga mwamba na mabeki wa Somalia waliokoa kabla ya kipa Mwadini Ali naye kufanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju wa Aden Hussein, kabla ya dakika ya 85, Aggrey Morris kupachika la tatu kwa kichwa akiunganisha kona ya Khamis Mcha.
Hadi mwisho wa mchezo, Zanzibar 3 Somalia bila. Kwa ushindi huo, Heroes imepenya hadi robo fainali baada ya kufikisha pointi nne na kukamata nafasi ya pili Kundi B nyuma ya vinara Uganda, ambao katika mechi ya pili hiyo jana

Comments