ZAMALEK WAANZA KUIFANYIA UKACHERO YANGA

ZAMALEK
Na Dina Ismail
WAPINZANI wa Yanga katika ligi ya mabingwa  barani Afrika Zamalek ya Misri imeanza kuingiwa tumbo joto dhidi ya wapinzani wao katika ligi hiyo Yanga, imefahamika.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam mapema wiki hii  zinaeleza kwamba tayari Zamalek imetuma makachero wake nchini kuanza kuwapeleleza wapinzani wao.
Kama hiyo haitoshi, Zamalek imeshaanza kusaka kanda za michezo mbalimbali iliyocheza Yanga katika siku za hivi karibuni ili kuweza kuzifanyia kazi.
Mmoja ya wadau wa soka kutoka nchini Misri aliliambia gazeti hili kwamba, tangu Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) litoe ratiba yao, uongozi uliaamua kuingia msituni ili kuweza kuwasoma wapinzani wao.
“Yaani huku hawa watu matumbo joto wanahaha huku na kule kutafuta taarifa za Yanga na kujua wataweza vipi kuwakabili,”Alisema mtoa taarifa huyo.
Taarifa zinaongeza zaidi, Wamisri hao wameamua kusaka rekodi ya Yanga baada ya kuvuliwa ubingwa kwa mara ya mwisho na mahasimu wao Simba mwaka 2002.
Yanga na Zamalek zitaanza hatua ya awali ya michuano hiyo kwa kucheza kati ya Februari 17 na 19 nchini Misri  kabla ya kurudiana Machi 2 na 4.

Comments