ZAMALEK KITU GANI BANA -YANGA

YANGA imejinasibu kutowahofia wapinzania wao katika ligi ya Mabingwa barani Africa (CAF) Zamalek ya Misri na kusema kuwa si lolote kwao.
Yanga itakayoanza hatua ya awali ya michuano hiyo kwa kucheza nyumbani kati ya februari 17 na 19 imesema watu wamekuwa wakiwasifu sana Wamisri hao kuwa ni mwiba mchungu kwa timu za Tanzania lakini kwao haiwaumizi kichwa.
"Zamalek kitu gani bana, kikubwa ni maandalizi ya kutosha na ushirikiano baina ya viongozi, wachezaji, wanachama na hata wadau wote wa Yanga kwa hilo naamini mambo yatakuwa safi".
Kwa hapa Tanzania ni Simba pekee ndiyo iliyopata kuvunja mwiko wa kuivua ubingwa ZAmalek pale ilipoiutoa mwaka 2003.

Comments