YAYA TOURE NDIYE MWANASOKA BORA WA AFRIKA 2011

KIUNGO wa Ivory Coast   Yaya Toure (28) ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2011 kupitia  tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) na kufanyika  katika ukumbi wa Banquet uliopo ndani ya Ikulu ya  Ghana.
Toure anayekipiga katika klabu ya Manchester City ya Uingereza  alitwaa tuzo hiyo  baada ya kupata kura nyingi   na kuwapiku nyota wenzake aliotinga nao fainali, Mghana  Andre Ayew na  Seydou Keita wa Mali .
Mbali na tuzo hiyo pia kulitolewa tuzo mbalimbali kama ifuatavyo:
Mchezaji bora wa mwaka (anayekipiga Afrika):
 -Oussama Darragi (Tunisia).
Mchezaji  bora (Wanawake)
- Perpetua Nkwocha (Nigeria)
Mchezaji anayechipukia:
- Souleymane Coulibaly (Ivory Coast)
Mwamuzi bora:
-Noumandiez Doue (Ivory Coast)
Kocha Bora:
-Harouna Doula (Niger)
Timu bora ya Taifa (Wanawake):
-Cameroon
Klabu bora:
- Esperance  ya Tunisia)
Nidhamu ya Mchezo:
-Libya
Tuzo ya Heshima:
-Mustapha Hadji( Morocco) na Austin ‘Jay-Jay’Okocha ( Nigeria)

Kiungo wa Ivory Coast, Yaya Toure (katikati), wa Manchester City, akipokea tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2011 mjini Accra, Ghana kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Globacom, Adewale Shangowawa (kulia). Toure mwenye umri wa miaka 28, aliwapiku kiungo Mghana wa Marseille, Andre Ayew (wa pili kushoto) na kiungo wa Mali na Barcelona, Seydou Keita katika kura zilizoopigwa na makocha wea Afrika.

Comments