YANGA KUISAKIA MAKALI ZAMALEK AFRIKA KUSINI

KATIKA kuhakikisha inawatoa magwiji wa soka barani Afrika, Zamalek ya Misri, mabingwa wa soka nchini , Yanga wamepanga kwenda kupiga kambi nje ya nchi sambamba na kucheza mechi za kirafiki za kimataifa.

Yanga itakuatana na Zamalek katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo itacheza mechi yake ya hatua ya kwanza nyumbani kati ya Februari 17 na 19 nyumbani kabla ya kurudiana Machi 2 na 4, mwaka 2011.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga amesema  kwamba moja ya nchi iliyopendekeza na benchi la ufundi kwenda kuweka kambi ni Afrika Kusini.

Comments