WAZIRI NCHIMBI AZINDUA RASMI KAMATI YA VAZI LA TAIFA

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitaka kamati maalum ya kupendekeza Vazi la Taifa kutimiza wajibu wake ipasavyo ili kukamilisha mchakato huo kwa muda uliokusudiwa. Waziri Nchimbi alisema hayo leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati alipoizindua rasmi kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga. “Napenda niwaaeleze wananchi kwamba sikukurupuka kuteua wajumbe wa kamati hii, nilipata ushauri toka kwa watu mbalimbali.Wajumbe mnayokazi kubwa sana kwani ni lazima tufike mwisho na tuwape Watnaznia kile ambacho wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu na baada ya kupatikana vazi mtasaisdia kulitangaza ili wananchi walijue,”Aliongeza. Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kusaga pamoja na kushukuru kwa kuteuliwa huko, alisema kamati yake itafanya kazi hiyo kwa nguvu zote kuhakikisha vazi hilo linapatikana. Mbali na Kusaga kamati hiyo inaundwa pia na Angela Ngowi (Katibu), Habibu Gunze, Bibi.Joyce Mhaville, Bw.Mustafa, Hassanali, Absaloom Kibanda, Makwaiya Kuhenga na Ndesambuka Merinyo ambao ni Wajumbe

Comments