WATANZANIA TUMEVUNA TULICHOPANDA-JULIO


KOCHA Msaidizi wa timu ya taifa ya Bara 'Kilimanjaro Stars' Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa kuvuliwa ubingwa wa Cecafa Chalenji  kwa timu hiyokulitokana na uadui mkubwa ulioibuka tangu mwanzo ambapo baadhi ya Watanzania walikuwa wakiizomea timu hiyo ilipokuwa ikiicheza na kuzishangilia timu pinzani.
Kili Stars ilivuliwa ubingwa juzi na Uganda katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kutandikwa mabao 3-1, katika mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Comments

  1. Hana lolote.
    Kama ninaulizwa mimi kwanini tumevuna hicho tulichovuna basi nitatoa jibu rahisi tu ni kwasababu yake Julio.
    Julio ndo aliyetuharibia team,na yeye ndo anyestahili kubeba lawama zote.
    Anapaswa kufahamu kuwa team ya Taifa ya Tanzania Bara tena inayoshiriki mashindano ya kimataifa ni tofauti na team ya mkoa wa kisoka ya Ilala inayoshiriki Taifa Cup,wakati kwenye Taifa Cup wapinzani wanatoka Lindi na Rukwa kwenye Challenge wapinzani wanatoka kwenye mataifa yenye mikakati endelevu ya Soka kama Uganda,Rwanda na Sudani.
    Anajua kabisa kuwa team inakwenda kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa badala ya kufanya selection ya maana yeye analeta ushikaji,ushikaji kwenye uchaguaji wa team,ushikaji kwenye ufundishaji,ushikaji kwenye upangaji wa team,unategemea nini? tena ashukuru vipaji binafsi vya wachezaji wachache to mention but few Ngassa,Kazimoto na Nurdin ndo vilivyotusaidia hadi tukapenya kwa huo mgongo wa best looser otherwise tulikuwa tunatia fora ka aibu katika mashindano yale,Jamaa Bw**e sana,anaacha kufanya kazi aliyopewa na TFF kwa niaba ya Watanzania wote kwa ufasaha anabwabwaja hovyo kwenye media,is he a proffesional kweli,mi nafikiri TFF wangehakiki carrier yake,I doubt

    ReplyDelete

Post a Comment