WASO MUKENYA WAIBUKIA COASTAL UNION

NYOTA wa zamani waliopata kutikisa katika klabu za Simba na Yanga, Mkenya Edwin Namiti Mukenya na Mrundi Ramazan Waso ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na klabu ya Coastal Union ya Tanga kwa ajili ya kuitumikia kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wakali hao ambao wamesajiliwa kama wachezaji huru, wataungana na wapya wengine waliosajiliwa na timu hiyo katika dirisha dogo wakiwemo Felix Ameche na Samuel Temi (Nigeria), Ahmed Shiboli  (Simba), Lameck Dayton (Villa Squad ), David Changula (Azam FC), Laurent Mugia, Mugenzi Philipo na Bakari Mohamed (huru).
Aidha, timu hiyo imewatoa kwa mkopo katika timu tofauti akiwemo, Omari Hamis aliyepelekwa Kwarara FC ya Zanzibar inayoshiriki ligi daraja la pili,Konji Yohana, Abdallah Ulasi na Ramadhan Nyumbi waliopelekwa AFC Arusha na Omari Maligwa (Morani SC).
Kajma hiyo haitoshi, timu hiyo imewatupia vilago wachezaji, Yahaya Akilimali, Juma Salum, Sabri Makame, Abdallah Abasi,Hassani Banda na Farouq Ramadhani.

Comments