WAAMUZI 14 BONGO WAVIKWA BEJI ZA FIFA


Waamuzi 14 wakiwemo wawili wapya wamefanikiwa kupata beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2012 baada ya kufaulu mtihani wa waamuzi uliofanyika mwaka huu na kusimamiwa na shirikisho hilo.
Ferdinand Chacha na Ali Kinduli ambao ni waamuzi wasaidizi ndiyo wapya katika jopo hilo la waamuzi wa FIFA kwa Tanzania. Waamuzi wa kati waliopata tena beji hizo ni Ramadhan Ibada, Orden Mbaga, Israel Mujuni na Sheha Waziri.
Mbali ya Chacha na Kinduli, waamuzi wengine wasaidizi kwa upande wa wanaume ni Josephat Bulali, Hamis Changwalu, Erasmo Clemence, Khamis Maswa na Samuel Mpenzu. Kwa upande wa wanawake, mwamuzi wa kati ni Judith Gamba wakati wasaidizi ni Mwanahija Makame na Saada Tibabimale.
Mwamuzi pekee wa FIFA 2011 ambaye jina lake halikurudi ni John Kanyenye ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi.



13 WASHIRIKI KOZI YA UKAMISHNA
Kozi ya siku mbili ya ukamishna iliyomalizika Desemba 29 mwaka huu imeshirikisha washiriki 13 chini ya ukufunzi wa Stanley Lugenge, Leslie Liunda na Sunday Kayuni.
 
Walioshiriki kozi hiyo ni Abdallah Zungo, Ally Mkomwa, Ally Mozi, Army Sentimea, Awadi Nchimbi, Beatus Manga, Christopher Mpangala, Hakim Byemba, Josephat Magazi, Juma Mgunda, Juma Mpuya, Mugisha Galibona, Ramadhan Mahano, Robert Kalyahe na Said Nassoro.
 
Wakufunzi wanaendelea kusahihisha mitihani ya washiriki na baada ya kazi hiyo kwa ambao watakuwa wamefanya vizuri majina yao yataingizwa katika orodha ya makamishna kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano mengine yanayosimamiwa moja kwa moja na TFF.
 

Comments