UPASUAJI KUMUWEKA YEPES NJE YA DIMBA KWA WIKI 10

MLINZI wa AC Milan  Mario Yepes atakuwa nje kwa wiki kumi kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu wake wa kulia ambayo yatamfanya afanyiwe upasuaji.
Yepes alipatwa na majeruhi hayo katika mechi baina ya AC MIlan na Bologna jumapili iliyopita na timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 na hivyo kutolewa kabla ya mchezo kumalizika.
Kwa mantiki hiyo  walinzi wa nyuma ambao wataendelea kuliendesha jahazi Milan  inayoshiriki ligi ya Seria A ikishika nafasi ya tatu ni pamoja na Alessandro Nesta, Thiago Silva na  Philippe Mexes.

Comments