UGANDA YAIVUA UBINGWA WA CHALENJI KILI STARS

TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanajro Stars' imeutema rasmi ubingwa wa CECAFA Chalenji baada ya kufungwa mabao 3-1 na Uganda katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulipigwa kwa dakjika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1, hivyo kulazimika kwenda dakia 30 nyingine ambapo katika dakika hizo Stars ilitandikwa mabao mawili.
Kwa mantiki hiyo, Kili Stars sasa itasaka nafasi ya tatu kwa kucheza na Sudan, huku Uganda itakwaana na Rwanda 'Amavubi'

Comments