TULIPANGA KUMSIMAMISHA BASENA-TFF

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limeshangazwa na kitendo cha aliyekuwa kocha wa Simba, Mganda Moses Basena kufanya kazi nchini bila ya kuwa na vyeti vya taaluma ya ukocha kwa kipindi chote cha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara alichoitumikia klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema kuwa walikuwa mbioni mbioni kumsimamisha Basena kocha kwani alikuwa akifanya kinyume na sheria za nchi pamoja na kanuni za shirikisho hilo.
Alisema kuwa waliwasiliana na Simba kwa zaidi ya mara tatu wakiomba kuwasilisha vyeti vya kocha huyo lakini wakashindwa kufanya hivyo na wakiwa mbioni kumsimamisha ndipo Simba ikaamua kumtupia virago.
“Sisi hatuna utaratibu wa kutoa adhabu, tunachokifanya ni kuwasailian ana pande husika na pindi inaposhindikana ndyio tunaamua la kufanya ikiwemo hilo la kutoa adhabu,”Alisema.
Simba ilitangaza kumtema BAsena kutokana na kutokuwa na vyeti vya taaluma yake na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na kocha aliywahi kuifundisha timu hiyo mwaka juzi, Mserbia Milovan Cirkovic ambapo tayari Simba imeshawasilisha vyeti vyake TFF.

Comments