TFF YAWAPOTEZEA BOBAN, TAITA


LICHA ya kudai kuwa inasubiri ripoti toka kwa benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kuhusina na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyofanywa na wachezaji wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' na Godfrey Taita, limeshindwa kutoa tamko ama hatua ilizowachukulia wachezaji hao.
Hatua hiyo inafuatia nyota hao kuonyesha utovu wa nidhamu katika kambi ya timu hiyo wakati wa michuano ya michuano ya CECAFA Chalenji 2011 iliyomalizika nchini Desemba 10.
Ilidaiwa kuwa wakiwa kambini, Boban aliondoka kambini bila ya ruhusa ya viongozi wake, huku Taita akidaiwa kuingiza mwanamke chumbani kwake.
Mmoja ya viongozi wa kamati ya nidhamu ya TFF alisema kwamba itakuwa ni vigumu kuwaadhibu wachezaji hao kutokana na ukweli kwamba hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.


Comments