TENGA NA WENZAKE KUWANIA LESENI B YA UKOCHA INAYOTAMBULIWA NA CAF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha majina ya makocha 40 wa Tanzania kushiriki katika kozi ya ukocha ya leseni B ya shirikisho hilo. Makocha wote waliopitishwa wana cheti cha ukocha cha ngazi pevu (advance).
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ni miongoni mwa makocha hao watakaoshiriki kozi hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 19-22 mwaka huu.
Wengine na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa (Dar es Salaam), Michael Bundala (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), John Simkoko (Morogoro), Juma Mwambusi (Mbeya), Samson Mkisi (Mbeya) na Sylvester Marsh (Mwanza).
Salum Madadi (Dar es Salaam), Mohamed Nyange (Dodoma), Madaraka Bendera (Arusha), Ally Mtumwa (Arusha), Charles Mkwasa (Dar es Salaam), Idd Mshangama (Dar es Salaam), Hassan Mlwilo (Dar es Salaam), Mohamed Msomali (Morogoro), Mbarouk Nyenga (Tanga) na Leopard Mukebezi (Dar es Salaam).
Mohamed Tall (Dar es Salaam), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam), Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Oscar Korosso (Mbeya), Charles Kilinda (Pwani), Fred Minziro (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Kagera), Hamimi Mawazo (Mtwara), Rogasian Kaijage (Kagera), Eugene Mwasamaki (Dar es Salaam) na Mohamed Mozi (Tabora).
Charles Matoke (Dar es Salaam), Peter Magomba (Singida), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Juma Nsanya (Tabora), Jamhuri Kihwelo (Dar es Salaam), Gilbert Mahinya (Tabora), Juma Mzigila (Morogoro), Joseph Sehaba (Dodoma), Charles Mngodo (Dodoma) na Mohamed Rishard (Dar es Salaam).


Boniface Wambura MgoyoOfisa Habari


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHDecember 8, 2011 at 5:04 AM

    MBONA SIJAONA JINA LA MICHAELA WAMBURA HAPO??

    ReplyDelete

Post a Comment