SIMBA YAPIGWA 3-2, YAENDA ZANZIBAR

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Simba SC jana kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi, Mbagala mjini Dar es Salaam walifungwa mabao 3-2 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara. Mabao ya Mtibwa yaliwekwa kimiani na Thomas Maurice dakika ya 61, Yussuf Nguya kwa penalti dakika ya 68 na Kessy Bingula dakika ya 72, wakati ya Simba yalifungwa na Ramadhan Singano dakika ya 61 na Felix Sunzu dakika ya 86. Baada ya kipigo hicho, Simba inatarajiwa kuondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo kesho  watafungua  dimba na Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan visiwani humo.

Comments