SIMBA WAENDA KUFANYA UKACHERO RWANDA

WEKUNDU wa Msimbazi Simba Sc imetuma makachero wake nchini Rwanda ili kwenda kusaka taarifa za wapinzania katika kombe la Shirikisho, Kiyovu ya nchini humo, imefahamika.
Timu hizo zinatarajiwa kukutana februari 17 na 19 kabla ya kurejeana Machi 2 na 4.
Kiongozi mmoja wa Simba alikiri kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovick na mjumbe wa kamati ya Utendaji, Ibrahim 'Maestro' wamekwenda Kenya kwa ajili ya kusaka mikanda ya timu hiyo ili kuweza kuifanyia kazi kabla ya kukabiliana nao.

Comments