RAIS WA ZANZIBAR,DK.SHEIN KUKABIDHI MWALI MABINGWA WA CECAFA CHALENJI 2011

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kufunga michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Sherehe za ufungaji wa mashindano hayo yaliyoshirikisha mataifa 10 wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na timu mbili mwalikwa zitafanyika Desemba 10 mwaka huu baada ya mchezo wa fainali utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments