PAPIC AHOFIA MASHINDANO

WAKATI Yanga ikikabiliwa na michuano kadhaa katika siku za hivi karibnuni,  kocha wake mkuu, Kostadin Papic anaonekana kuhofuia ushiriki wa timu yake katika michuano hiyo.
Yanga ambayo wiki ijayo itaanza kwa kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi kabla ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara na klabu biongwa ya Afrika, kwa sasa ipo katika maandalizi yanayoonekana ya kusuasaua.
Kwea mujibu wa Papic ambaye mapema wiki hii 'alipasua jipu' kuhusiana mambo yalivyo ndivyo sovyo ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam, itakuwa ngumu kwa timu yake kufanya vema katika michezo hiyo kutokana na maandalizi duni.
Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwqa mazoezi lakini si ishara ya timu kuwa tayari kwa mashindano na anampango wa kukutana na viongozi wa timu hiyo ili kuweka mambo hadharani.
Ikumbukwe kuwa, kocha huiyo ambaye amerejea siku chaache kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara, kabla ya kutimka kwake Yanga amekuwa akihofia timu yake kushiriki mashindano ama mechi kadhaa za kirafiki kwea sababu anazozijua mwenyewe. 

Comments