OKWI KUIKAMILISHA SIMBA LEO

MSHAMBULIAJI wa kimataifa ya Simba, Mganda Emmanuel Okwi anatarajiwa kurejea nchini leo, imefahamika.
Nyota huyo alikwenda kwao kwa ruhusa maalum ili kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa ambayo huadhimishwa Desemba 25 kila mwaka.
Ujio wa Okwi utakamilisha kikosi cha timu hiyo ambacho kinaendelea na maandalizi yake katika viwanja vya TCC Chang'ombe chini ya kocha wake mkuu, Mserbia Milovan Cirkovic.

Comments