Tanzania (Ngorongoro Heroes) imeanza kwa sare michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa vijana chini ya miaka 20 inayofanyika Gaborone, Botswana.
Jana (Desemba 2 mwaka huu) katika mchezo dhidi ya mabingwa watetezi Zambia uliofanyika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Gaborone, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 3-3.
Mabao ya Ngorongoro Heroes yalifungwa dakika ya 2 na 13 kupitia kwa Simon Msuva. Bao la tatu lilifungwa na Hassan Dilunga dakika ya 40. Evans Kangwa aliifungia Zambia mabao mawili wakati la kusawazisha lilifungwa na Alex Sichone.
Ngorongoro iliwakilishwa na; Jackson Wandwi, Hassan kKessy, Issa Rashid, Samuel Mkomola, Frank Raymond, Atupele Jackson, Simon Msuva, Amani Kyata, Edward Shija, Frank Sekula na Hassan Dilunga.
Tanzania itacheza mechi ya pili Desemba 4 mwaka huu na Afrika Kusini wakati ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Desemba 6 mwaka huu dhidi ya Mauritius.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments
Post a Comment