NIYONZIMA, MICHO WACHANUA TUZO ZA CECAFA CHALENJI

                                                                          HARUNA NIYONZIMA
                                                                                       MICHO
WAKATI michuano ya CECAFA Chalenji ikifikia tamati leo, baraza hilo limewatangaza wateule wa vipengelea mbalimbali ambapo kocha aliyepata kuifundisha timu bingwa ya ligi kuu soka Tanzania Bara, Sredojevic Milutin 'Micho' ambaye katika michuano alikuwa akikinoa kikosi cha Rwanda 'Amavubi'alitangazwa kuwa kocha bora wa mashindano.
Aidha, kipa wa Sudan,  Elmoiz Maghroub wa Sudan alitwaa tuzo ya kipa bora,wakati mshambuliaji wa Rwanda, anayekipiga katika klabu ya Yanga,  Haruna Niyonzima alitwaa tuzo ya mchezaji bora na Wiish Yabarow Somalia mwamuzi bora wa mashindano hayo.
Aidha, mgeni rasmi katika fainali hizo, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein alikabidhi  Kombe, medali ya dhahabu na kitita cha dola 30,000 kwa mabingwa wa mwaka huu, Uganda,wakati Rwanda iliyokuwa ya  pili ilijipatia dola 20,000, kombe na medali za fedha na Sudan iliyoshika nafasi ya iliondoka na  medali ya shaba na dola 10,000.

Comments