NGORONGORO HEROES WAANZA KAZI COSAFA LEO



TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, leo inatarajiwa kuanza kutupa karata yake ya kwanza katika michuano ya Shirikisho la Soka Nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA), kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Botswana jijini Gaberone.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, Ngorongoro itaumana na Zambia ambapo timu hizo zimepangwa Kundi C.
Wambura alisema Ngongoro inayonolewa na Kocha Mdenish Kim Poulsen akisaidiwa na Adolph Rishard itashuka dimbani majira ya saa 12.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Mbali ya Ngorongoro Heroes na Zambia, timu nyingine katika kundi hilo la C ni Afrika Kusini na Mauritania.

Comments