MR.EBBO AFARIKI DUNIA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abel Motika 'Mr. Ebbo' amefarikia dunia usiku wa kuamkia leo.
Taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa msanii huyo ambaye alikuwa pia mmiliki wa studio ya Motika Records, alikutwa na umauti baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Msanii huyo atakumbukwa kwa mengi kwani enzi za uhai wake alijipatia umaarufu wa kuimba nyimbo zake kwa kutumia lafudhi ya kimasai, huku akitamba na nyimbo kama 'Kamongo', Me Mmasai', 'Fahari Yangu' na nnyinginezo.
Mipango ya mazishi inafanywa, Mwenyezi mungu ailaze pema roho ya marehemu, Amin.

Comments