MILOVAN APIGWA STOP NA UHAMIAJI, WALUSIMBI ATUA SIMBA


KOCHA wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic amezuiwa na Idara ya Uhamiaji kutokana na kutokuwa na kibali na cha kufanya kazi nchini na sasa uongozi wa Simba unakwenda mbio kuhakikisha unampatia kibali.

Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage alisema jana kwamba uongozi wa klabu yake unafanya jitihada za haraka kuhakikisha Msetrbia nhuyo anaopata kibali na kuanza kazi rasmi.  

Katika hatua nyingine, Simba imemnasa beki wa kushoto wa Uganda, Godfrey Walusimbi na atajiunga na Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ujio wa Walusimbi, ambaye anahesabiwa miongoni mwa mabeki bora wa kushoto katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni wazi utawapa presha mabeki wa sasa wa timu hiyo, Amir Maftah na Juma Jabu, ambao wamekuwa wakipokezana nafasi hiyo katika kikosi hicho cha Msimbazi.

Maftah ni majeruhi kwa muda mrefu, sasa Jabu anatamba kwenye nafasi hiyo.

Walusimbi sasa ameamua kujiunga na Simba baada ya kufanya majaribio katika nchi za Sudan na Ethiopia.

Baada ya kukwama kupata timu huko, alirudi Uganda na kujiunga na Bunamwaya, ambako mkataba wake unamalizika baada ya miezi mitatu.

Simba walicheza karata yao wakati wa Kombe la Chalenji na kumshawishi Walusimbi kujiunga nao.

Walusimbi ambaye alicheza mechi zote za CECAFA Tusker Challenge akiwa amevaa jezi namba 15, alisema; “Naipenda Simba na ndiyo klabu yangu ninayokuja kuichezea msimu ujao,”alisema.

“Nimeshafanya mazungumzo na viongozi wao ninachosubiri ni kumalizia mkataba wangu na Bunamwaya na baada ya hapo, nitakuwa huru kukamilisha mambo yangu,” alisema Walusimbi.

Comments