MILOVAN APATA KIBALI UHAMIAJI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

               Kheri na Fanaka ya Mwaka Mpya.

KLABU ya Simba ina furaha kuutangazia umma kwamba Kocha Mkuu wake, Profesa Milovan Cirkovic, leo amepata kibali cha kufanya kazi nchini.

Klabu inapenda kutumia nafasi hii kushukuru Idara ya Uhamiaji, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali kwa ujumla kutokana na ushirikiano wa hali ya juu ulioonyeshwa katika kipindi cha kushughulikia suala hili.

Kwa taarifa hii, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu, wanatoa wito kwa wadau, washabiki na vyombo vya habari kumpa nafasi Milovan ili sasa apate fursa ya kuutumia ujuzi wake wa hali ya juu kwenye kuimarisha soka la Tanzania.

Ikumbukwe kuwa kwa leseni yake ya ukocha alionayo, Milovan ndiye atakuwa kocha wa kiwango cha juu zaidi anayefanya kazi nchini kwa sasa.

Simba inaomba ushirikiano kwa wadau wote hao.

MECHI YA SIMBA NA ESKOM YA MALAWI

MECHI hii ambayo awali ilipangwa kuchezwa siku ya Krismasi (25 Dec) sasa imeahirishwa hadi Jumanne (26 Dec) ijayo.

Mabadiliko haya yametokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam ambazo zimeathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya watu, wakiwamo wapenzi wa kandanda na pia Uwanja wa Taifa wenyewe ambako mechi ilipangwa kuchezwa.

Kwa tangazo hili, Simba pia inapenda kutoa salamu za pole kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika na mvua hizo za Dar, Mar na Mbeya.

Klabu ya Simba iko pamoja na wote ambao wameguswa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba Sports Club
                                     0772 01 72 47                                              

Comments