MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA, KILI YAAHIDI ZAWADI YA UBINGWA CHALENJI

KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS

KOCHA msaidizi wa timu ya Taifa ya Bara 'Kilimanjaro Stars' Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameahidi kutoa zawadi ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwa Watanzania kwa timu hiyo kuibuka na ushindi wa michuano ya CECAFA Chalenji 2011, inayoendelea katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Julio amejinasibu ya kuwa pamoja na timu yake kutokuwa na matokeo mazuri sana katika mechi zake lakini si sababu ya kuwafanya washimndwe kutetetea ubingwa huo na matokeo yake wamekuwa wakipata miujiza.
"Ili mtu uwe tajiri lazima uwe na historia kwani hata Bakhressa ni tajiri lakini alianza kama mshona viatu,"ALisema Julio.
Kilimanjaro Stars ambayo inatetea ubingwa huo imetinga hatua ya nusu fainali ambapo kesho itakwaana na Uganda kwenye hatua hiyo.

Comments