MAN UNITED YAPIGA 5-0, CITY YASHIKWA 0-0

Mshambuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov akiwapigia makofi mashabiki wakati akitoka uwanjani baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Wigan Athletic, Uwanja wa Old Trafford, Manchester.

Kiungo wa West Bromwich, Paul Scharner (kushoto) akichuana na kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (kulia) katika mechi ya Ligi Kuu ya England  juzi kwenye Uwanja wa The Hawthorns, West Bromwich, West Midlands, England. Timu hizo zilitoka 0-0.

Kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa ameketi kwenye benchi akifuatilia mechi kati ya timu yake na Blackburn Rovers Uwanja wa Anfield, Liverpool. Timu hizo zilitoka 1-1.

Comments