MAFARAO WAOMBA KUCHEZA NA STARS

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limepokea maombi toka Misri ikiomba mechi ya kirafiki kati yao na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katia ya Februari 23 na 24, 2012, nchini Misri.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osia amesema kwamba wamepokea mwaliko huo na wameshakubali ombi hilo na kwamba gharama za usafiri na malazi na huduma zote litakuwa juu ya wenyeji wao.

Comments