KONGAMANO VIJANA WA YANGA KESHO



NAIBU Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dk.Fenera Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la Vijana wa Yanga linalotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa PTA Sabasaba.

Mratibu wa kongamano hilo, Kais Edwin amesema maandalizi yanakwenda vema ambazo zaidi ya watu 3500 watashiriki katika kongamano hilo litakalojadili mambo mbalimbali.

Baadhi ya mada zitakazijadiliwa na pamoja na vijana wa timu hiyo kujitambua kama sehemu ya mchango wao ndani ya klabu, pia jinsi ya kuanzisha vitega uchumi ambavyo vitaweza kuisaidia klabu hiyo.

Kama hiyo haitoshi pia watajadili uanzishwaji wa Saccos yao ambapo maazimio yote yatapelekwa kwa viongozi wa Yanga

Comments