KILI STARS YAFUZU NA MANUNDU CHALENJI

LICHA ya kutandikwa mabao 2-1 na Zimbwabwe, timu ya soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CECAFA Chalenji 2011.

Kili ambayo imeingia hatua hiyo kama ‘Best Looser’ wa kundi A baada ya kufikisha pointi tatu ilizozipata kupitia mechi zake kwenye mnichuano hiyo hivyo itakutana na Malawi jumanne katika hatua hiyo.
Kabla ya mechi hiyo, kulifanyika mchezo wa kundi C baina ya Sudan na Kenya ambapo Sudan iliitandika Kenya bao 1-0 na hivyo kutinga Robo fainali hivyo kesho itapepetana na Burundi katika hatua hiyo.
Aidha, Zanzibar ambayo imetinga robo fainali kama ‘Best Looser’ itakwaana na Rwanda.

Comments