KARUME KUFUNGUA MAPINDUZI CUP

RAIS mstaafu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Abeid Aman Karume, anatarajiwa kufungua rasmi michuano ya kombe la Mapinduzi itakayoanza kurindima Januari 2, 2012 katika Uwanja wa Aman Visiwan Zanzibar.
Katika ufunguzi huo utakaofanyika usiku, Ma bingwa w2a Ligi Kuu Bara Yanga watakwaana na Mafunzo ya Zanzibar, huku Azam na Kikwajuni wataanza mashindano hayo katika mechi itakayopigwa saa kumi jioni.
Mashindano hayo ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatazikutanisha timu nane zikiwemo pia mabingwa watetezi Simba, Zanzibar Ocean View.

Comments