K-LYN AUPA KISOGO MUZIKI

MWANAMUZIKI  wa kizazi kipya nchini Jacquiline Ntuyabaliwe maarufu kama 'K-Lyn' ameamua rasmi kuachana na muziki na kuendeleza nguvu katika fani ya upambaji.
K -Lyn ambaye alipata kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania 2000 amesema kwamba kutokana na kufanya sanaa hiyo ya muziki kwa muda mrefu, ameona aachane nayo na kujikita katika shughuli hiyo ya upambaji wa kumbi na ushauri wa masaula ya upambaji.
"Nilianza kuimba tangu nikiwa nina miaka 17,  nadhani nimetumika vya kutosha katika fani hii, hivyo nimeona niachane nayo na kuangalia mambo mengine ikiwemo kazi yangu hii ya sasa ya upambaji,"Alisema.
Mrembo huyo ambaye alichipukia katika bendi ya Tanzanite na baadaye kusahiriki mashindano ya urembo, baada ya kuwa msanii wa kujitegemea alipata kutoka na singo kadhaa zilizoweka matawi ya juu sambamba na kumpatia tuzo ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya singo za K-Lyn zilizopata kuwashika ni pamoja na 'Best', 'Nikipata Wangu', 'Crazy Over U', 'Nipe Mkono', 'Chochote Utapata' na nyinginezo. 

Comments