JAMA MBA AOMBEWA ITC CAMEROON


Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Robert Jama Mba ambaye ni raia wa Cameroon ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili acheze soka nchini humo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetuma maombi hayo jana (Desemba 5 mwaka huu) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kupata hati hiyo.

Mba ambaye aliichezea Yanga enzi za uongozi wa Imani Madega ameombewa ITC kwa ajili ya kujiunga na klabu yake ya zamani ya Tiko United baada ya mkataba wake ndani ya Yanga kumalizika.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na ITC itatolewa wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika.

Comments