HUZUNI TENA, MPIGANAJI JOHN NGAHYOMA HATUNAYE TENA

TASNIA ya habari nchini imepata pigo jingine leo baada ya mtangazaji mkongwe, John Ngahyoma (pichani) kuaga dunia usiku wa kuamkia leo nchini India.
Ngahyoma ambaye alikuwa akipiga mzigo katika shirika la Utangazaji la BBC alikutwa na umauti huo katika hospitali moja nchini humo alipokuwa akipata matibabu.
Enzi za Uhai wake, marehem,u alipata kufanya kazi nchini katika mashirika mbalimbali ikiwemo IPP Media akitangaza katika kituo cha Televisheni cha ITV.
Kifo cha Ngahyoma kimezidi kuumiza mioyo ya Wanahabari na Watanzania kwa ujumla kwani ni jana tu tulimpoteza dada yetu mpendwa, Halima Mchuka ambaye anazkwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu Halima na John mahala pema peponi, Amin.

Comments

  1. DADA DINA, JOHN AMEFARIKI NYUMBANI KWAKE TABATA SEGEREA SAA MOJA NA NUSU ASUBUHI NA SIO NCHINI INDIA.

    ReplyDelete

Post a Comment