GOR MAHIA YAICHOMOLEA SIMBA

GOR MAHIA

KLABU ya Gor Mahia ya Kenya imefuta mpango wake wa kucheza mechi ya kirafiki na vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba.
Timu hizo zilitarajiwa kucheza mechi hiyo mwezi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ushiriki wake wa kombe la Shirikisho (CAF) mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Kenya zilizotumwa kwa uongozi wa Simba na mmoja ya viongozi wa Gor Mahia, Martha Enok, wameamua kuachana na Simba baada ya kutaka dau kubwa.
Kiongozi huyo alieleza katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala kwamba klabu yake haitaweza kumudu kiasi cha fedha ilichohitaji Simba ili kwenda huko.
“Kweli tuliialika Simba ili Kenya tucheze nayo mechi ya kirafiki lakini tumeona tuachane nao baada ya kutangaza dau kubwa la fedha ili kuweza kuja,”Alisema Martha.
Hata hivyo, hakuna kiongozi yoyote wa Simba aliyepatikana kuzungumzia suala hiyo baada ya kutopatikana kwa njia ya simu ya kiganjani.
Wakati Simba itaanza hatua ya awali ya kombe la Shirikisho kwa kucheza na Kiyovu ya Rwanda kucheza ugenini,Gor Mahia itaanza hatua hiyo kwa kucheza na Ferroviario de Maputo ya Msumbiji ambapo mechi za kwanza zitapigwa kati ya Februari 17 na 19 kabla kurudiana Machi 2 na 4.

Comments