FABREGAS, KIIZA WATIMKA YANGA

                                                                                         NIYONZIMA
KIIZA
WAKATI mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga wakiendelea na maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa,mabingwa hao imewapa mapumziko nyota wake  wawili wa kimataifa wa klabu ya Yanga, Mrwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas' na Mganda Hamis Kiiza.
 Nyota hao wamekwenda kwao kwa mapumziko mafupi baada ya kuzitumikia timu zao za Taifa zilizokuwa zikishiriki mashindano ya CECAFA Chalenji 2011 yaliyomalizika nchini Jumamosi iliyopita na Uganda kutwaa ubingwa.

Comments