EMMANUEL MAISHA KILANGI:MCHEZAJI ALIYEFUNGWA LIBYA KUTOKANA NA HILA ZA WAKALA, AELEZA UCHAFU WANAOUFANYA MAWAKALA WA SOKA


Na Dina Ismail


UKIWAONA ama kusikia mikakati yao katika kusaka mafanikio ya soka huwezi kuamini, kama ndiyo hao wanaodumaza ama kutaka kuua mchezo huo kwa ajili ya manufaa yao.
Ndiyo, ni kwa manufaa yao kwa sababu watu hao wanajulikana kama  mawakala wa wachezaji nchini, baadhi yao wamekuwa wakitumia uwakala huo kwa ajili ya kujinufaisha wao na si wachezaji.
Emmanuel Maisha Kilangi ni mmoja ya wachezaji ambaye amekumbana na mitihani mingi ya kimaisha ikiwemo kufungwa jela nchini Libya iliyotokana na kuingizwa ‘kingi’ na wakala mmoja (jina kapuni) ambaye alitaka kumtumia kwa manufaa yake.
Mchezaji huyo anaweka wazi kuwa mchezo unaofanywa na mawakala hao ambao baadhi yao hujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ndiyo unapelekea wachezaji wengi wa Kitanzania ambao wanagoma kuifanya kupotezwa nje ya mipaka ya nchi .
Jan 2010 alipelekwa nchini Libya mwezi Januari 2010 ambapo alifanya majaribio katika klabu ya daraja la kwanza , Har Du na kufauli, hata hivyo wakala wake alimtaka kuachana nayo kwa madai ya kumtafutia timu nchini Sweden.
Akiwa nchini Libya akiishi katika mji wa Tripol alikuwa akipata huduma zote tyoka kwa Watanzania kadhaa ambao wapo karibu na wakala huyo ambapo baada ya muda ndipo mambo yakaanza kwenda ndivyo sivyo ambapo wenyeji wake walianza kumshawishi ajikite katika mtandao wao wa kusafirisha dawa za kulevya.
Wenyeji hao walimtaka abebe mzigo kupeleka nchini Mauritius na kumuahidi kumpa fedha nyingi pindi atakapofanikisha, lakini aligoma kutokana na ukweli kwamba biashara hiyo ni haramu na pia alikwenda huko kusaka maisha kihalali (soka).
Kutokana na kugoma huko, wenyeji hao wakaanza kumtishia kumchomea kwa idara ya uhamiaji ya huko, kabla ya wakala aliyempeleka naye kwenda na kumshawishi lakini Emmanuel alisimama katika msimamo wake , matokeo yake alichoma moto pasi yake ya kusafiria.
Kama hiyo haitoshi wakala huiyo alikwenda kumchomea Uhamiajia kuwa ni Mrundi anaishi isivyo halali nchini humo, hivyo maofisa usalama walimchukua na kumpeleka polisi kabla ya kufungwa kwa miezi sita.
Baada ya kuachiwa mwezi januari mwaka huu alikabidhiwa kwa balozi wa Burundi nchini humo ambapo balozi huyo alimsafirisha hadi nchini Burundi na kufikia kiambi moja ya wakimbizi iliyopo eneo la Manyovu, Bujumbura.
Kutokana na maisha ya kambini kuwa magumu alikuwa akijushughulisha na kazi ya kuchimba mawe na kuyauza, huku akitafuta njia ambayo itamuwezesha kutoka nchini humo na kurudi Tanzania.
Kwa bahati nzuri katika pilikapilika zake alikutana na dada mmoja mfanyabiashara ambaye baada ya kuongea naye na kuona na anamoyo kweli wa kumsaidia alimsimulia masahibu yaliyomkuta, hivyo dada huyoa libenba jukumu la kumsaidia.
Hata hivyo, katika msaada wake huo alikumbana na vishawishi vya dada huyo kumtaka kimapenzi huku akitaka ampe ujauzito tu, lakini alikuwa akigoma kujihusisha na masuala hayo, mwisho wa siku alialazimika kuwa na uhusiana na dada huyo na kubahatika kutimiza matakwa yake.
“Kweli nilikuwa nahudumiwa kila kitu na yule dada hata kiasi cha kunipa nisimakjie miradi yake huku pia akitaka nimuoea, lakini nyumbani ni nyumbani hivyo nilimdanga nya nakiuja kufatilia ITC na huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kurejea huku”, Anasema.
Anasema akiwa huko alipata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya Rayon na kufaulu lakini suala la kibali likawa tatizo na hivyo baada ya kurejea nchini mwezi Mei alipiga hodi TFF lakini baada ya kueleza tu mkasa aliokumbana nao,hakuweza kupata ushirikiano tena toka kwa watendaji wa chini wa shirikisho hilo.
Kutokana na kutopata msaada wowote toka TFF mchezaji huyo amejikuta akiishi katika mazingira magumu ambapo katika harakati zake za kusaka nauli ya kurudi kwao, Makamu Mwenyeki wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alimpatia kiasi cha fedha.

Comments