DIAMOND ADONDOSHA PINI JIPYA 'NIMPENDE NANI'



WAKATI sakata la msigano wa kimapenzi baina ya msanii nyota wa muziki wa bongo fleva Nassib Abdul ‘Diamond’ dhidi aliyekuwa mpenzi wake Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa, Jokate Mwegelo likiendelea kushika kasi, msanii huyo ameachia singo mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nimpende Nani’.
Diamond ametoa singo hiyo kama swali kutokana na hali halisi ya sakata hilo inavyoendelea kwa sasa kwani wiki chache zilizopita aliachia singo nyingine mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mawazo’ ambao ndo kwanza umeanza kushika kasi katika vituo mbalimbali vya redio.
Wimbo huo ambao Diamond anaonekana kuujiuliza ampende nani kati ya wapenzi wake hao huku akiwataja kwa majina Wema na Jokate, huku singo hiyo ikiwemo ndani ya albamu yake aliyoingiza sokani mwezi Novemba iitwayo ‘Lala Salama’ ambapo sehemu ya mashairi ya wimbo huo inasema ““Yasiwe kama Wema sepetu kila siku kwenye magazeti, simtaki kama Uwoya ni mtemi anahasira,awe mpole kama Jokate…nimpende nani, nimpendeee”.
Mbali na wimbo huo mpya, albamu hiyo inanyimbo kama Moyo Wangu ambao ulipata kushika chati mbalimbali za muziki, pia kuna Lala salama uliobeba jina la albamu, Chanda chema, Nimpende nani, Najua,Mawazo,Kwanini,Gongolamboto,Natamani na Kizaizai.
Awali Diamond ambaye alipata kutwaa tuzo tatu za muziki za Kilimanjaro, awali alitoa albamu ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Mbagala’ ikiwa na nyimbo kadhaa ambazo zilipata kufanya vema kwqenye medani za muziki zikiwemo Nalia na Mengi, Kamwambie, Nitarejea, Binadamu Wabaya na nyinginezo
.

Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHDecember 18, 2011 at 5:08 AM

    utoto unamsumbua..kalishwa perege antangaza mji nzima eti kala samaki je akilishwa pweza si matangazo yafika mpaka cnn...

    ReplyDelete

Post a Comment