CHALENJI YACHELEWESHA PROGRAMU ZA PAPIC

KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Mserbia Kostadin Papic ameshindwa kuanza progamu rasmi ya kukinoa kikosi chake kutokana na michezo ya Chalenji kuendelea.
Papic amelazimika kusubiri michezo hiyo kutokana na wachezaji wake kadhaa kuzitumia timu za taifa zinazoshiriki michuano hiyo.
Yanga imeshaanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo tangu wiki iliyopita ambapo wachezaji wa ndani na nje ya nchi ambao hawamo katika michuano ya Chalenji ambayo itafikia tamati jumamosi  wanaendelea kujinoa.

Comments