BUNGE FC YAWATOTESHA WAWAKILISHI FC


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Mwinyi Haji Makame akikabidhi kombe la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kwa Amos Makalla Nahodha wa Timu ya Soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Timu hiyo iliilaza timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar,bao 4-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam jana. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL), Teddy  Mapunda, Mkurugenzi wa Masoko, Ephraim Mafuru na meneja wa vinywaji vikali,Emilian Rwejuna.
Mechi hiyo ni sehemu ya shamra shamra za maadhiumisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, mechi iliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Comments